Sambaza

AMBER LULU ATAMBA KUMNG’OA SARAH KWA HARMONIZE

MWANAMUZIKI wa kike anayefanya vizuri kwenye anga la Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ ametamba kumtoa mchumba wa mkali kutoka kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), Rajab Abdulhan ‘Harmonize’, Sarah Michelotti endapo ataonesha udhaifu.

Awali, chanzo kilicho karibu na msanii huyo kilieleza kuwa, Amber amekuwa na ukaribu wa hali ya juu na msanii huyo kiasi kwamba lolote linaweza kutokea endapo nafasi itapatikana.

“Amber Lulu msimuone hivyo tu, anapenda sana kila kitu kutoka kwa Harmonize na kuna kipindi alisema atafanya juu chini ili Sarah akae pembeni na yeye ndio awe mama mjengo kwa sababu anampenda sana sana mwanamuziki huyo,” kilisema chanzo hicho.

Kama hiyo haitoshi, chanzo hicho kiliendelea kueleza kuwa, mara nyingi Amber anapenda sana kujichanganya WCB kwa ajili tu ya kuwa karibu na Harmonize.

Baada ya ubuyu huyo kutua gazetini, Ijumaa liliamua kumtafuta Amber Lulu ambapo alipopatikana aliweka wazi kuwa Harmonize ni mshkaji wake wa karibu lakini lolote linaweza kutokea.

Stori: MWANDISHI WETU, IJUMAA

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey