Sambaza

EXCLUSIVE: TANASHA AFUNGUKIA KUMWAGANA NA DIAMOND!

DAR ES SALAAM: Yamezungumzwa mengi na bahati mbaya mhusika hakupata haki ya kupewa fursa ya kusikilizwa kwa ukamilifu hivyo Amani limejipa jukumu hilo.

Ni juu ya habari nyingi za mchumba wa ‘taifa’ wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna Oketch ambaye mapema wiki hii ‘alitrendi sana’ kwenye mitandao ya kijamii akidaiwa kumwagana na jamaa huyo.

Hayo yote yalikuja kufuatia Diamond ‘kum-unfollow’ (kumuondoa kwenye kundi la marafiki wake kwenye mtandao wa Instagram) Tanasha na kudaiwa kurejesha majeshi kwa mama mtoto wake, Hamisa Mobeto kisha kumrejesha tena Tanasha.

Madai mengine yaliyowekwa mezani ni juu ya maelewano hafifu kati ya Tanasha na mama mzaa-chema (mama Diamond), Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ na familia hiyo kwa jumla hivyo kutakiwa kuchukua chake mapema kabla hayajamfika ya Zarinah Hassan na ‘maeksi’ wengine wa jamaa huyo.

TANASHA LIVE NA AMANI

Katikati ya mambo hayo mazito yaliyokosa ufafanuzi kwenye mitandao hiyo ya kijamii, Amani lilizungumza ‘live’ na Tanasha akiwa jijini Mombasa nchini Kenya anakofanya kazi katika Kituo cha Redio cha NRG ambapo alifungukia ishu hizo, kubwa likiwa ni kuachana na Diamond au Mondi.

TANASHA AMWAGIWA MADAI YOTE

Katika mahojiano hayo kati ya Amani na Tanasha ambaye pia ni mwanamuziki aliyeachia Wimbo wa Radio, mwanadada huyo alimwagiwa madai yote kama ifuatavyo;

Amani: Mambo vipi Tanasha? Hapa ni Amani. Kuna mambo mengi yamekuwa yakiendelea mitandaoni kubwa likiwa ni ishu ya wewe kuachana na Diamond, nini kinaendelea? Je, ni kweli mmeachana?

Tanasha: Napenda kuwaambia watu wasiamini kila wanachokiona kwenye mitandao ya kijamii hasa kwenye hizi kurasa za udaku na umbeya.

D (Diamond) na mimi sasa hivi tupo vizuri sana tena sana kuliko wakati mwingine wowote.

Au ni kwa sababu hatupostiani mitandaoni kama mwanzo? Hiyo haimaanishi kuwa kuna tatizo, hakuna tatizo. Tuna sababu zetu wenyewe.

Amani: Vipi kuhusu madai mengine ikiwemo ishu ya wewe kuwa na ujauzito wa Diamond?

Tanasha: Nimekueleza kwamba watu wasiamini kila wanachokiona kwenye mitandao ya kijamii hasa kwenye hizi kurasa za udaku na umbeya. Asante!

BABA DIAMOND

Kwa upande wake baba Diamond, Abdul Juma alipozungumza na Amani hivi karibuni kuhusu mwanaye huyo, alisema anamuunga mkono kwa mkwewe wa sasa (Tanasha) japo pia anamkubali sana Mobeto.

“Yani namkubali Tanasha awe mkwe wangu kama watakuja rasmi lakini pia Mobeto. Ikiwezekana kwa vile dini inaruhusu, anaweza akawaoa wote tu,” alisema Baba Diamond.

TUMEFIKAJE HAPA?

Madai ya Tanasha kuachana na Mondi yamekuwepo kwa muda mrefu tangu jamaa huyo alipoahirisha ndoa yao waliyopanga kuifunga Februari 14, mwaka huu.

Uhusiano kati ya Tanasha na Diamond kila kukicha umekuwa ukigonga vichwa vya habari tangu walipouanzisha mwishoni mwa mwaka jana.

Hata hivyo, uhusiano huo umekuwa na wakosoaji wengi kwenye mitandao ya kijamii kutokana na warembo ambao Diamond alitembea nao kabla ya Tanasha.

Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Mwijaku ni mmoja wa watu waliowahi kumfungukia Tanasha kuwa asichukulie kitendo cha kutambulishwa kwa wazazi wa Diamond kuwa ndiyo tayari amepata kibali cha kuolewa kwani staa huyo wa Wimbo wa Inama siyo muoaji na ameshawadanganya hivyo warembo kadha wa kadha kama Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Mobeto, Wema Sepetu, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na wengineo.

“Kutambulishwa siyo ndoa, jiulize wangapi wametambulishwa kwa mama yake Diamond na hawakuolewa?

Huu ni utamaduni wetu Waafrika, ukitaka kuuteka moyo wa mwanamke mtambulishe kwa wazazi wako kisha utampata na ukishapata ulichokitaka na ahadi inaishia hapo,” alisema Mwijaku.

WENYEWE MAHABA NIUE

Hata hivyo, wenyewe Tanasha na Mondi wamekuwa wakioneshana mahaba niue kila wanapokutana mwishoni mwa wiki kwani wanaishi mbalimbali, Tanasha akiwa Mombasa, Kenya na Mondi akiishi Dar, Tanzania.

Stori: Sifael Paul, Amani

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey