T.I AKANUSHA TAARIFA YA KIFO CHA DADA YAKE
Baada ya TMZ kuripoti taarifa zakifo cha Precious Harris’62 ambaye ni dada wa Rapper T.I kimetajwa kuwa alizidisha matumizi ya dawa za kulevya aina ya cocaine ambapo ilipelekea kuongezeka kwa mapigo yake ya moyo na kusababisha kupata ajali mbaya ya gari. Saa chache T.Ialiamua kuongea kupitia Instagram LIVE na kuwasema vibaya TMZ na alikanusha taarifa hizo ambazo zilichapishwa na aliendelea kudai kuwa hakuna ukweli wowote juu ya taarifa hiyo na amesikitishwa na mtandao huo kuandika taarifa hiyo.T.I alingia kwenye ukurasa wake wa IG na kuandika ujumbe kwa dada yake.Pumzika kwa amani dada, tupo pamoja na wewe, silaha zinawezwa kutengenezwa lakini hawatoshinda sio leo. Ulikua mtu mwema kwa sisi wengi hatuwezi kuona kitu kinakudhuru au kukuweka kwenye hatari au vitu ulivyoacha” >>>aliandika T.I
Precious Harris’62 alifariki February 22,2019 baada ya kupata ajali mbaya ya gari huku vyombo vingine vya habari viliripoti kuwa alipoteza fahamu na kuanguka chini alipokuwa kwenye chumba cha kupigia simu na alikimbizwa hospitali ya serikali na kuripotiwa kufariki wiki moja baadae.