CHRIS BROWN AFUNGULIWA SHTAKA LA UBAKAJI
MTANDAO wa The Blast umeripoti kuwa mwanamuziki Chris Brown ameshtakiwa kwa kosa la kutotoa taarifa kamili kwa mwanamke anayedai kumbaka nyumbani kwake mjini Los Angeles miezi kadhaa iliyopita baada ya mwanamke huyo kumfungulia shtaka la ubakaji.

Kwa mujibu wa nyaraka za Mahakama mwanamke huyo Jane Doe alifungua file lenye maswali na kuitaka Mahakama kumuuliza Chris Brown kuhusu namba za simu alizokuwa akizitumia tokea tukio hilo February 2017 mpaka sasa kutokana na yeye kushindwa kupata jibu baada ya CB kumjibu kuwa ni swala binafsi na swali hilo halihusiani na kesi inayoendelea.

Chris Brown amezidi kukana shtaka hilo la ubakaji na kusema hakuna kitu kilichotokea nyumbani kwako huku Jane Doe akiamini kuwa endapo CB atakabidhi namba alizokuwa akitumia basi kutakua na ushahidi wa kutosha na amedai kuwa CB amekabidhi taarifa nusu.