Sambaza

NOTORIOUS B.I.G MTAA WAPEWA JINA LAKE

MAMA mzazi wa marehemu Notorious B.I.G   ameweka wazi kuwa mji wa New York umeamua kumpa heshima mwanae kutokana na mchango mkubwa alioutoa kwenye game ya muziki wa Hip Hop pamoja na mtaa aliokuwa anaishi.

Notorious B.I.G ambaye alifariki miaka 22 iliyopita amepewa moja ya mtaa na kuitwa jina lake, Ms. Voletta ameeleza kuwa mtaa huo utaitwa ‘Christopher Wallace Way’ na umezinduliwa rasmi June 10,2019 katika makutano ya barabara ya St James Place na mtaa wa Fulton Brooklyn Marekani.

Notorious B.I.G ambaye jina lake halisi ni Christopher Wallace alizaliwa May 21, 1972 New York Marekani na kufariki March 9 1997 kwa kupigwa risasi na enzi za uhai wake aliacha ngoma kibao ikiwemo One more chance, Dead Wrong, Juicy, Who shot Ya na nyingine nyingi.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey