Sambaza

KHLOE KARDASHIAN AWEKA WAZI MAHUSIANO YAKE YALIYOPITA…

MWANAMITINDO Khloe Kardashian aweka wazi mahusiano yake yaliyopita na mchezaji wa kikapu wa NBA Tristan Thompson na amafunguka sababu kubwa iliyomfanya kuingia kwenye mahusiano hayo ni baada ya kuambiwa kuwa Tristan aliachana rasmi na aliyekuwa mpenzi wake.

Khloe Kardashian aliandika ujumbe huo kupitia kwenye insta story baada ya kuwepo na tuhuma kuwa mpenzi wa zamani wa Tristan ambaye ni Jordan Craig kudai kuwa mpenzi wake alianzisha mahusiano mengine na Khloe kipindi akiwa mjamzito na kudai kuwa alimuuliza Tristan kuhusu tetesi hizo lakini alikana.

“Ukweli ni kwamba Nilikutana na Tristan na aliniambia kuwa ameachana na mpenzi wake na alinionyesha mpaka uthibitisho hata mama yake mzazi alinithibitishia hilo niliamini hicho, naomba sana msamaha kama Tristan na watu wake walidanganya kuhusu hilo, Mungu anajua naomba na kutoka moyoni naomba msamaha kwa maumivu ambayo yamejitokeza hakuna mwanamke ambaye anastahili kupitia wakati mgumu, huu ndio ukweli wangu” aliandika Khloe
Jordan Craig alibahatika kupata mtoto wa kiume pamoja na Tristan Thompson mwaka 2016 na April 12,2018 Khloe Kardashian na Tristan walipata mtoto wa kike ambaye anafahamika kwa jina la True Thompson hata hivyo Khloe Kardashian na Tristan waliachana rasmi mwezi February mwaka huu.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey