Sambaza

Utajiri Mchumba Wa Ben Pol Usipime

DAR ES SALAAM: Kama ulikuwa hujui, habari ikufikie kwamba, mchumba wa staa mwingine wa Bongo Fleva, Benard Michael Paul Mnyang’anga ‘Ben Pol’, Anerlisa Muigai ana utajiri si wa nchi hii, Ijumaa limeuchimba na kuuweka kibindoni wote! 

Kupitia mitandao mbalimbali ambayo Gazeti la Ijumaa limemchimba mrembo huyo na kubaini kuwa utajiri wake wa jumla unasoma Dola za Kimarekani bilioni moja (zaidi ya shilingi trilioni 2.3).

ANAWAACHA MBALI ZARI, REGINA

Kwa mantiki hiyo, mrembo huyo mwenye umri wa miaka 31 anakuwa amewaacha mbali mno kama mbingu na ardhi ‘mabosi ledi’ wengine ambao walikuwa wakiaminika kuwa na mkwanja mrefu Afrika, mwanamama Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, raia wa Uganda na Regina Daniels ambaye ni mwigizaji mwenye jina kubwa nchini Nigeria.

TUMTAZAME ZARI KIDOGO

Zari mwenye umri wa miaka 38 ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa Afro-Pop barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, anayeishi Afrika Kusini, anatajwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani milioni 4.4 (zaidi ya shilingi bilioni 10) Utajiri wa Zari unatokana na maduka pamoja na vyuo vya urembo anavyomiliki mrembo huyo mwenye asili ya Uganda.

REGINA NAYE

Regina mwenye umri wa miaka 18 ambaye ameolewa na mfanyabishara mkubwa nchini Nigeria, Ned Nwoko, kabla ya kukutana na mumewe huyo bilionea, anatajwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani 350,000 (zaidi ya shilingi milioni 800).

Mrembo huyo ambaye kwa siku za hivi karibuni kufuru zake zimekuwa gumzo mitandaoni kwa kuonekana hata kumfunika Zari kutokana na kuonekana akiwa na magari ya kifahari na ndege yake binafsi, naye anaonekana kuachwa mbali zaidi na Anerlisa.

Regina ni prodyuza na mwigizaji nchini Nigeria ambapo tofauti na kazi yake ya uigizaji, umaarufu wake umechagizwa zaidi baada ya kuolewa na kigogo huyo ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wa kutosha.

TURUDI KWA ANERLISA

Mbali na biashara nyingine ndogondogo, Anerlisa utajiri wake umetokana na kampuni yake ya maji inayofahamika kwa jina la NERO. Kampuni hiyo inatajwa kuwa inaongoza kwa usambazaji wa maji nchini Kenya.

AMEFUNDISHWA NA MAMA’KE

Mrembo huyo amefundishwa biashara angali akiwa na umri mdogo na mama yake, Tabitha Karanja ambaye ni mmiliki wa kampuni kubwa ya bia iitwayo Keroche Breweries ya nchini Kenya. Kampuni hiyo ya bia ndiyo kampuni kubwa inayoongoza kwa kuuza vinywaji mbalimbali vyenye kilevi nchini humo.

Licha ya kuwa kwenye familia yao wako vizuri kifedha, vyanzo mbalimbali vinaeleza mitandaoni kuwa, Anerlisa hakutaka kuitegemea familia yake, lakini alipambana kutafuta za kwake.

Jarida la Forbes limemtaja mrembo huyo kuwa miongoni mwa vijana 40 wa barani Afrika wenye utajiri mkubwa ambao pia wanatarajiwa kuwa matajiri zaidi siku zijazo. Maji ya mrembo huyo ndiyo yanayoongoza kwa mauzo katika supermarket zote na maduka nchini Kenya.

UTITIRI WA MAGARI

Mbali na kumiliki mijengo ya kifahari jijini Nairobi nchini Kenya, mrembo huyo anatajwa kumililiki magari kibao ya kifahari yakiwemo Range Rover Sport, Mercedes Benz na mengineyo ambayo yanayazidi yale ya Zari anayotamba kwa kuyaandika majina yake.

PENZI LAKE NA BEN POL

Mrembo huyo alikutana na kuanzisha uhusiano na Ben Pol mwaka jana baada ya jamaa huyo kwenda kufanya shoo nchini humo na penzi lao likaota mizizi hadi kufikia hatua ya kuvalishana pete ya uchumba.

Akizungumza na gazeti hili la Ijumaa, Ben Pol aliyeachia wimbo wake mkali mpya wa Wapo mapema wiki hii alisema kuwa anamshukuru Mungu kumkutanisha na mrembo huyo ambaye wanaelewana na mambo yakienda sawa, atafunga naye ndoa.

ANASEMAJE KUHUSU UTAJIRI WA MCHUMBA’KE?

Kuhusu utajiri wa mchumba’ke huyo, Ben Pol alisema ni kweli mwenza wake huyo ana utajiri mkubwa unaotokana na biashara zake halali.

REKODI YA WABONGO KENYA

Ben Pol anakuwa miongoni mwa wasanii kadhaa kutoka kwenye Bongo Fleva ambao wamepata wanawake kutoka nchini Kenya. Kwenye orodha hiyo yupo Diamond na Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey