Sambaza

Juma Sharobaro Atamani Kumshirikisha Janjaro

BONGO Fleva imenoga! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya raia wa kigeni kuonesha makeke yao! Wakati Msambaa wa Norway, Igrid Fossum ‘Makihiyo’ akikamua katika muziki huu, yupo mwingine Mzaramo wa Msanga, Tang Jing ‘Juma Sharobaro’ ambaye jana alitinga ndani ya Studio za +255 Global Radio, Sinza Mori jijini Dar kutambulisha ujio wake mpya.

Juma Sharobaro Akiwa ndani ya Studio za +255 Global Radio, Alipokuja Kutambulisha Nyimbo yake Mpya

Akizungumza katika kipindi cha Bongo 255, Juma Sharobaro ambaye kiasili ni Mchina, anatamba na Wimbo wa Cha Upepo ambapo ndani ya video hiyo amesema ingependeza kama msanii mwenzake, Dogo Janja angehusika kama Video King.“Kabla sijaachia wimbo huu, nilishawahi kuzungumza na wengine kama Master Jay kwenye nyimbo zangu lakini pia Dogo Janja, nilitamani kumchukua awe Cha Upepo kwenye video yangu kwa sababu nilishawahi kumuona amejiremba kwenye wimbo wake mmoja,” alisema Juma Sharobaro.

.. Akiwa Ndani ya Ofisi ya Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho

Juma Sharobaro alizungumza mengi katika mahojiano yake ikiwemo namna alivyolipata jina lake.
“Wakati najifunza Kiswahili walimu wetu walitupatia majina mengi na kulikuwa na bahati nasibu ya karatasi, kulikuwa na majina ya Juma, Said na Aziz nikachagua Juma. Ukija kwenye Sharobaro ni mtu mtanashati mwenye kiduku kama mimi. Nilinyoa nywele hivi kwa muda mrefu kwa hiyo nazisifia sana nywele hizi, kiduku, kijogoo ama kibwezi,” alimaliza kusema Juma Sharobaro.

Juma Sharobaro ambaye pia ni Meneja Mkuu wa Masoko wa StarTimes Tanzania mahojiano yake yanapatikana moja kwa moja kupitia Youtube kwa jina la Global TV Online. Pia unaweza kusikilizaa Global Radio kwa kupakua APP yenye jina la 255 Global Radio katika Playstore kwenye simu yako.

Imeandaliwa na Andrew Carlos/ GPL

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey