Sambaza

Baghdad aeleza alivyomtoa Nandy, Rayvanny na Whozu

RAPA tishio Bongo, Praygod Kweka ‘Baghdad’ ameeleza namna alivyokutana na mastaa wa Bongo Fleva na kuwatoa kimuziki kipindi wakiwa hawajulikani. Baghdad anayetikisa kwa sasa na Ngoma ya Tangazeni iliyosukwana Prodyuza Lorenzo wa Sinza Music aliiambia +255 Global Radiokupitia kipindi cha Bongo 2555 kuwa, kabla ya Nandy kuwa msanii alimjua kutokana na mkewe.

“Nandy ni rafiki wa mke wangu na alikuwa anatumika kutoaushauri kipindi nataka kumuoa mke wangu, pia alikuwakiniomba ushauri wakati anataka kutoka kimuziki nikamwambiaunajua kuimba lakini sema hujajua utumikaje hivyonikamshirikisha kwenye wimbo wangu wa…akatokea hapo,” alisema Baghdad na kuongeza.

“Nilikuwa mtu wa kwanza kumtafuta na kumwambia unaweza,akaniambia anaenda chuo lakini tulihangaika na akaja Dar na garila magazeti akaja na kutokea hapo.

“Upande wa Rayvanny niliwahi pia kumwambia una uwezomkubwa sana na siku watu wakiutiliamaanani utakujakuniambia,” alimaliza kusema Baghdad.

Mbali na kufanya mahojiano hayo, Baghdad alikuwaameongozana na Daktari Hassan Mwamba Masoud kutoka KhalaliHerbal Clinic ambayo inajihusisha na mambo ya Tiba Asili na Mbadala.

“Karibuni Khalali Herbal Clinic pale Magomeni Mwembechai Mtaa wa Kimambea na Itungi tunatoa huduma nyingi ya kusaidia jamii vijana kama Baghdad ambao walikuwa na uzito mkubwa.

“Pia tunatibu Kisukari, vidonda vya tumbo, bawasiri na UTI sugu na dawa zetu ni za asili hazina kemilikali yoyote. Kumbuka kwamba huduma zetu ni nzuri na hatuangalii pesa bali kutibu
kwanza,” alisema Daktari Hassan.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey