Sambaza

Mwili Wa Dada Wa Shigongo Alivyoagwa Bupandwamhela

Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo akiongea jambo.

MWILI wa dada wa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global Group, Eric Shigongo, marehemu Vaileth James Bukumbi, umeagwa na kuzikwa leo Ijumaa, Juni 21, 2019, nyumbani kwao katika Kijiji cha Bupandwamhela, Buchosa – Sengerema mkoani Mwanza.

 

Akitoa neno la Shukrani, Shigongo aemsema; “Nachukua nafasi hii kuwashukuruni sana kwa kujitoa maisha yenu kwa ajili ya familia yetu. Nashukuru kwa wema mliotuonyesha. Nimesimama hapa kwa niaba ya ndugu zangu, mmeacha shughuli zenu kuja kutufariji.

“Nimesimama hapa kando ya jeneza la dada yangu Vaileth, nilikuwa nampenda sana dada yangu na nitaendelea kukupenda, nakumbuka wakati unachumbiwa ulichumbiwa na wanaume watatu lakini mimi nilikushauri uolewe na James ambaye alikuwa maskini, mlitafuta naye mali mkapata, ulikuwa mpambanaji sana, kupoteza mtu kama huyu ni hasara kubwa sana

“Nakumbuka yapo hata baadhi ya matatizo mengine yalikuwa hayafiki kwangu, alikuwa anayamaliza yeye, nimejizuaia kabisa kulia kwa sababu yenu nyie ndugu zangu mliokuja hapa nyumbani kutupa faraja. Nasema asanteni kwa kutupenda na hamchoki kwa kushirikiana na sisi.

“Mambo haya ni kama saa, haya tunayoyapitia ni msimu tu. Sisi tunamcha Mungu na yeye ni kila kitu kwetu. Hatufikirii kingine bali tunaamini kwamba ni mipingago ya mungu. Mungu wa mbinguni atusaidie.

“Ni matajiri wengi wanakufa na kuwaacha matajiri, niwaombe ndugu zangu tuwajari wenye hali ya chini, wasionacho kwani tunajiwekea hazina, ninawapenda sana, na Mungu wa mbinguni awabariki.

“Vaileth ameungana na baba yangu, mama yangu, kaka yangu Julius, na dada yangu Jesca wametengeneza familia nyingine huko mbinguni, tunaamini ipo siku tutakutana nao na kuungana nao tena,” amesema Shigongo.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey