Sambaza

Gigy Money Acharuka Kuhusu Mwanaye, Ni Baada ya Mashabiki Kumkera

Msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’.

BAADA ya kuvuja video ikimuonesha akicheza na mwanaye, Mayra huku mashabiki wakimjia juu kuwa anamharibu, msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amecharuka kwa kusema kuwa atabaki kuwa mwanaye hata waseme vipi.

Juzikati kupitia ukurasa wake wa Instagram, Gigy aliposti kipande cha video akiwa na mwanaye wakicheza ambapo kwa mtazamo wa mashabiki walisema kuwa alikuwa akimharibu kutokana na staili aliokuwa akicheza naye.

Akizungumza na Shusha Pumzi, Gigy alicharuka kwa kusema; “Watu wengine sijui wakoje, mimi nashaangaa watu wamenitolea povu weee kwani hakuna mzazi ambaye anacheza na mwanaye? Mimi niliamua tu kucheza na mwanangu kama wengine wanavyofanya ila ndiyo kila mtu ana mtazamo wake sidhani kama kucheza kuna tatizo tena wanitue.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey