Sambaza

Wema Sepetu Aachiwa kwa Dhamana na Kupewa Onyo Kali

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Jumatatu, Juni 24, 2019 imemwachia kwa dhamana Malkia wa Filamu Bongo, Wema Sepetu baada ya kukaa mahabusu ya Segerea kwa siku saba tangu Jumatatu iliyopita, Juni 17 kwa kukiuka masharti ya dhamana yake.

Aidha, mahakama hiyo imemuonya Wema kwa kitendo chake cha kukiuka masharti ya dhamana na kumtaka kutorudia tena huku kesi yake ikitajwa kusikilizwa tena Julai 4, 2019.

Wema alionekana kuficha uso wake mara nyingi alipokuwa mahakamani hapo na baada ya kuachiwa kwa dhamana, aliwakwepa mapaparazi kwa kukimbia huku akipitia mlango wa nyuma wa mahakama hiyo ili asipigwe picha na wanahabari.

Wema anakabiliwa na mashtaka ya kujipiga picha za zisizo na Maadili na mpenzi wake kisha kuzisambaza kupitia mitandao ya kijamii.  Kupata Stories na Kusikiliza Exclusive Enterrviews na Wasanii Mbalimbali, Pakua App ya 255 Global Radio kwa Kubofya Hapa

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey