Sambaza

Kim Nana Wa Diamond Platnumz Atimuliwa Kwenye Nyumba Aliyokuwa Akiishi

MAJANGA! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mrembo Lilian Kessy ‘Kim Nana’ kudaiwa kufukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar, Gazeti la Ijumaa Wikienda limedokezwa.

TUJIUNGE NA CHANZO

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa Wikienda, mtu wa karibu wa mrembo huyo ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini alisema kuwa, Kim Nana ameondolewa kwenye nyumba hiyo aliyokuwa amepanga baada ya kushindwa kwenda sawa na baba mwenye nyumba.

“Hee! Ninyi hamna huu ubuyu? Mbona una karibu miezi mitatu tangu ametimuliwa? Fuatilieni kwa undani zaidi maana najua ninyi mnajua namna ya kuchimba vitu, lakini kikubwa ni kwamba walishindwana kwenye ishu ya kodi na baba mwenye nyumba,” aliweka nukta rafiki huyo.

MBEYA MWINGINE ANENA

Baada ya kumalizana na rafiki huyo wa Kim Nana, Ijumaa Wikienda lilimfikia jirani wa mrembo huyo ambaye naye alidai kuwa, Kim Nana alichemka kulipa kodi baada ya kufulia.

“Mimi niliona alivyokuwa anahama hapa, lakini nasikia alikuwa amefulia sasa mambo ya kodi yakawa yanasumbua ndiyo baba mwenye nyumba akaona isiwe taabu, amfukuze na kuweka mpangaji mwingine,” alieleza jirani huyo ambaye naye aliomba hifadhi ya jina.

IJUMAA WIKIENDA LATINGA NYUMBANI…

Baada ya kunyapianyapia kutoka kwa jirani na rafiki wa mrembo huyo anayeuza sura kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Gazeti la Ijumaa Wikienda liliamua kutinga moja kwa moja katika nyumba hiyo aliyokuwa anaishi Kim Nana.

IJUMAA WIKIENDA NA BABA MWENYE NYUMBA

Baada ya kufika nyumbani hapo, Ijumaa Wikienda lilifanikiwa kukutana na baba mwenye nyumba ayejitambulisha kwa jina moja la Raymond ambaye alithibitisha kumuondoa Kim Nana katika nyumba yake na kuweka mpangaji mwingine.

Mahojiano kati ya Mzee Raymond na Gazeti la Ijumaa Wikienda yalikuwa hivi;

Mzee Raymond: Karibuni sana.

Mwandishi: (Huku akijifanya hajui chochote) Asante! Tumekuja kumuangalia Kim Nana, lakini mlango wake umefungwa, atakuwa amekwenda wapi?

Mzee Raymond: Huyo binti aliondoka hapa miezi mitatu iliyopita, alishindwa kulipa kodi yangu hivyo nikaona bora aende tu kwa sababu mimi hapa nipo kwa ajili ya kutafuta pesa na siyo mambo mengine, (akasisitiza kwa kimombo) A’m here to make money).

Mwandishi: Lakini tumepata taarifa kwamba ulimfukuza.

Mzee Raymond: (Anacheka) wewe jua tu ameondoka kwa sababu alishindwa kulipa kodi yangu.

Mwandishi: Kwani kodi hapa ni shilingi ngapi mzee wangu?

Mzee Raymond: Ni shilingi laki mbili; chumba kinakuwa na vyumba viwili na choo ndani.

Mwandishi: Basi sawa baba tunashukuru.

Mzee Raymond: Haya karibuni tena.

IJUMAA WIKIENDA LAMCHEKI KIM NANA

Gazeti la Ijumaa Wikienda liliondoka nyumbani hapo na kumpigia simu Kim Nana ili kuweka mambo sawa ambapo baada ya kupatikana na kuelezwa kuwa gazeti hili limefika nyumbani kwake na kumkosa na kwamba alifukuzwa kwa kushindwa kulipa kodi, alishtuka!

“Hee! Jamani ndiyo yamekuwa hayo, halafu kwa nini mnaenda kwenye nyumba za watu bila kutoa taarifa? Kwa hiyo ndiyo

mmeambiwa nimefukuzwa kwa sababu ya kodi, makubwa,” alisema mrembo huyo na kukata simu, hata alipotafutwa kwa mara ya pili muda huohuo hakupokea.

TUJIKUMBUSHE

Kim Nana ni mmoja kati ya warembo ambao wamewahi kutoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambapo ni maarufu kwa jina la Kim wa Diamond au Kim wa Mondi.

Katika kipindi alichokuwa na jamaa huyo alikuwa kipenzi cha mama Diamond, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ kabla penzi lao kuota mbawa ndani ya muda mfupi.

ILIKUWA ABADILI DINI…

Mama Diamond a.k.a Mama Dangote aliwahi kukaririwa na gazeti dugu na hili la Amani kuwa tayari wameanza kumfundisha Kim Nana mafunzo ya Dini ya Kiislam ili aolewe, lakini ghafla upepo ukageuka, huku na huku mzee baba Diamond akarusha ndoana ikanasa kwa mrembo kutoka Kenya Tanasha Donna Oketch.

Baada ya muda mfupi kupita, Tanasha akatafakari kimtindo, akamuelewa Diamond, wakaweka mambo hadharani na ndiyo habari za Kim Nana zilipozikwa rasmi.

KWA SASA YUKO NA NANI?

Kim Nana kwa sasa inaelezwa kuwa ana uhusiano na mtangazaji wa East Africa Television, T-Bway.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey