Sambaza

Cheki Vibe La RosaRee Akitambulisha Ngoma Yake Mpya “CHAMPION”

RAPA wa kike aliye kwenye kiwango cha juu Bongo, Rosa Ree jana alitia maguu ndani ya Redio ya +255 Global na kuitambulisha ngoma yake mpya ya Champion.
Rosa Ree alifahamika zaidi kupitia ngoma yake ya kwanza iliyoitwa One Time akiwa chini ya Lebo ya The Industry iliyopo chini ya Nahreal, kisha akadondosha nyimbo zingine kadhaa kabla ya kuanza kujitegemea.

Akizungumzia Champion ambayo kamshirikisha Ruby, Rosa Ree alisema alipata wazo la kuandika wimbo huo kutokana na baadhi ya watu kuchukulia poa mafanikio ya mtu fulani pasipo kufikiria changamoto alizopitia hadi kuyafikia.

“Nilipata wazo la kuandika Wimbo wa Champion kama sehemu ya kuwashitua watu kuwa wasikate tamaa licha ya changamoto wanazozipitia, wote ambao wanahisi kuna milango ipo mbele lakini wanaona kama imefungwa,
Champion ya Rosa Ree yafika Global Radio wenye matatizo kwenye ndoa zao pia nataka kuwaambia wasikate tamaa.

“Hata yule ambaye amekuwa Champion,  amefanikiwa kuna wakati ilifikia hatua alikaribia kukata tamaa, kwa hiyo msikate tamaa hicho ndiyo kitu nilichotaka kuwaambia, karibu msikilize wimbo wangu wa Champion,” alimaliza Rosa Ree wakati akitambulisha wimbo huo.

Akizungumzia uamuzi wa kumshirikisha Ruby, Rosa Ree alisema: “Ruby ni msanii mwenye uwezo mkubwa sana wa kuimba, mimi nikimsikia akiimba live huwa nachanganyikiwa sana, kitu kingine ni mtu mwenye upendo na anakubali kazi zangu,” alisema Rosa.

Stori na  ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey