Sambaza

Filamu Ya R Kelly Yashinda Tuzo Mtv

FILAMU ya “Surviving R Kelly” iliyoachiwa rasmi Januari 3,2019 ya mkongwe wa muziki wa RnB Ro R Kelly imefanikiwa kushinda tuzo ya “Best Documentary” kwenye tuzo za filamu za MTV zilizofanyika hivi karibuni nchini Marekani.

Filamu hiyo ambayo iliibua maovu mengi ya mwimbaji huyo na kuchafua kazi yake ya muziki na kuibuka kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono kwa wanawake 10 waliokuwa chini ya umri wa miaka 18 ambapo R. Kelly alikanusha tuhuma hizo na kusema kuwa hazikua na ukweli wowote inatajwa kuangaliwa na watazamaji zaidi ya Mil.22 katika mtandao wa You Tube.

Inaripotiwa hadi sasa nguli huyo amefunguliwa mashtaka zaidi ya 11 ya unyanyasaji wa kingono pamoja na kuwekwa gerezani mara mbili huku ikielezwa kuwa watu wengi wamejifunza vitu vingi kupitia filamu hiyo ya ‘Surviving R Kelly”

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey