Sambaza

Marioo aitambulisha Inatosha Global, asimulia Dully alivyompa 500,000

HITMAKER wa Ngoma ya Chibonge, Omar Mwangaza ‘Marioo’ ametimba katika studio za +255 Global Radio ndani ya Global Group, Sinza Mori jijini Dar na kueleza ujio wake wa kishindo kupitia Ngoma ya Inatosha na Chibonge ambazo zinakimbiza kwa sasa.

Akifanyiwa mahojiano Bongo 255, Marioo ambaye ni msanii anayeongoza kwa kuwatengenezea mastaa wengi nyimbo kali ikiwemo Papa ya Gigy Money alisema kuwa, yeye na Hanstone walikuwa marafiki wakubwa chini ya Prodyuza Abbah

“Lakini baada ya Ngoma ya Iokote kufanya vizuri akaondoka kutokana na kutoelewana na uongozi. Baadaye Chibonge tulipotaka kuiachia (audio) walitaka kumtoa nikasema tumuache kwa kuwa ni ngoma ya wote na ni kali na vitu kama hivi vinaendaga kwa baraka. Baadaye video inataka kutoka nikamtafuta akasifia sana akasema ngoja akaongee na uongozi wake, sikudhani kama itashindikana kutokana na ukaribu niliokuwa naye.

“Baada ya wiki nikamtafuta tena, akashtuka akasema hawajampa jibu. Siku ikafika ya video, Hanstone akawa anaogopa. Abbah alikuwa tayari kumsamehe, tukamuita ofisini kwenye video hakutokea ikabidi nimtafute G Nako na kuingiza vipande vyake,” alisema Marioo.

Marioo pia aliongelea kipaji chake cha kuwaandikia mastaa mashairi kuwa, staa wa Bongo Fleva, Dully aliwahi kumsaidi sana.

“Sikuwahi kuwa na ndoto ya kuwaandikia watu mashairi. Nilikuwa nikirekodi ngoma studio kali, hadi Abbah akasema huyu dogo mkali kama kuna mtu atanisapoti yupo tayari. Kuna siku alimsikilizisha Dully nyimbo zangu akazikubali na kuniahidi kunisaidia, baada ya kukaa naye kwa muda kwenye studio yake naye akaniruhusu tena nikipata mwingine anisaidie lakini licha ya yorte, Dully aliwahi kunisaidia shilingi 500,000 niongezee kutengeneza video,” alimaliza kusema Marioo.

Marioo kwa sasa anatamba na vibao vingi kama Inatosha, Chibonge, Yale, Mboni Yangu, Waue na Ifunanya.

Mahojiano kamili tembelea Global TV Online kupitia Youtube au unaweza kupakua APP ya 255 Global Radio kupitia Playstore katika simu yako ya mkononi na kuweza kusikiliza vipindi vingi vya kijanja.
Imeandaliwa: Andrew Carlos/GPL

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey