Sambaza

T.I Akabidhi Tuzo Ya Nipsey Kwa Familia

RAPA Clifford Joseph Harris usiku wa kuamkia Jumanne, alikabidhi tuzo ya BET ya rapa mwenzake, marehemu Nipsey Hussle.  Katika tuzo hizo zilizotolewa ndani ya Ukumbi wa Microsoft Theater jijini Los Angeles, Nipsey ambaye licha ya kufariki amekuwa akikum-bukwa kwa kuwekewa alama mbali-mbali ikiwemo kinywaji cha Belaire Luxe, alikabidhiwa tuzo maalum ya Humanitarian na Lifetime Achievement.

Wakati wa kutolewa, T.I aliitwa maalum kukabidhi tuzo hiyo kwa familia ya Nipsey ikiongozwa na mpenzi wake, Lauren London na mama wa Nipsey, Angelique Smith. Akizungumza katika usiku huo, mama wa Nipsey alitoa maneno machache; “Nimeshangazwa kweli na upendo huu ambao ni wa duniani kote. Hata kama kimwili hatuko naye lakini kiroho bado tuko naye”

Naye Lauren alisema; “Naomba niwashukuru wote kwa upendo na sapoti yenu na sasa Marathon (duka la nguo aliloliacha Nipsey) linaendelea tena.” Nipsey pia katika usiku huo alishinda Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kiume wa Hip Hop.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey