Sambaza

Miss Kinondoni 2019 Yazinduliwa, Warembo Kuosha Magari (Picha + Video

BAADA ya kusubiriwa takribani mwaka mmoja, lile shindano maarufu Bongo la ulimbwende, Miss Kinondoni 2019 linatarajiwa kuzinduliwa  leo Juni 29, 2019 ndani ya viwanja vya The Life Club (Maisha Club), Mwenge jijini Dar ambapo warembo wameshiriki kuosha magari.

Akizungumza na +255 Global Radio Ijumaa Juni 28, 2019 kupitia kipindi cha Bongo 255, mratibu wa shindano hilo, Nancy Joseph ‘Supermodel’,  alisema uzinduzi wa shindano hilo utaanza mapema kuanzia saa 10:00 asubuhi hadi jioni na kutakuwa na burudani mbalimbali, nyama choma, kula na watoto yatima na pia kuosha magari.

“Karibuni sana kwa wingi katika uzinduzi huu. Warembo wote watakaoshiriki ambao ni 18 wataosha magari kwa wote watakaojitokeza nayo huku wakichaji shilingi 10,000 tu kwa gari.

 

“Pesa itakayopatikana hapo tutawapa watoto yatima wa Kituo cha Malaika. Warembo wataosha magari kwa wote watakaokuja tena watayang’arisha balaa,” alisema Nancy

Kilele cha Miss Kinondoni kitakuwa Julai 13, mwaka huu. Mwaka jana mshindi wa Miss Tanzania, Queen Elizabeth, alitokea Kinondoni.

Ili kupata mahojiano yote, tembelea Global TV Online katika Mtandao wa Youtube bila kusahau ku-subscribe. Pia unaweza kupakua APP ya 255 Global Radio kupitia Playstore katika simu yako ya mkononi.

 Imeandaliwa na: Andrew Carlos/GPL

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey