Sambaza

Cardi B awekewa Ngumu na Mamlaka za Marekani Kusajili Brand Yake

Mamlaka nchini Marekani imemtilia ngumu Cardi B kusajili Msemo wake wa ‘Okurrr’ Kuwa nembo yake ya Biashara (Brand). Rapper huyo hatoweza tena kutengeneza mkwanja kupitia msemo wake maarufu wa “okurrr,” imeripotiwa kuwa ombi lake la kuusajili msemo huo kama nembo ya biashara limepigwa chini na Mamlaka Husika nchini Marekani.

Mtandao wa Blast umeripoti kuwa juhudi za Cardi B za kuusajili msemo huo zimepiga mwamba kwasababu haujafikia vigezo vya kusimama kama nembo ya biashara na ni msemo ambao unatukimika kwa matumizi ya kawaida ya kila siku.

Pia imefahamika kuwa mashabiki wa Cardi B pia walishajaribu kuusajili msemo huo huo siku za nyuma lakini ombi lao lilipigwa chini pia.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey