Sambaza

Kylie Jenner, Bilionea Mdogo zaidi Duniani Azidi Kujitanua Kibiashara

Kylie Jenner (21) ametajwa na Jarida la Forbes hivi karibuni kuwa ndio Bilionea Mwenye Umri Mdogo kwa Hivi sasa.

Kylie ambaye ni mtoto wa Mwisho wa Chris Jenner na Bruce (Ambaye hivi sasa Amebadili Jinsia) na Kujiita Caitlyn Jenner ) amezidi kujiimarisha zaidi kibiashara kwa kuzidi kufungua Brands mpya za Biashara zake, Ukiachana na Kylie Hair, Kylie Cosmetics, Kylie Baby Mrembo huyo amefungua pia Biashara ya Vinywaji iitwayo ‘Kylie Booze’ ambayo itakuwa na bidhaa za vinywaji kama mvinyo wa wine, pombe, bia, vinywaji visivyo na vilevi pamoja na vinywaji vya kuongeza nguvu.

Kylie anayetoka katika familia ya Kardashian, akiwa ni mdogo wa Mwisho katika Familia ya Kina Kim Kadrshian anakadiriwa kuwa na Utajiri unaozidi dolla za Kimarekani Bilioni Moja. Licha ya kuzaliwa katika familia Maarufu sana Marekani na duniani kwa ujumla, Kylie pia amefanikiwa Kuwa na TV Show yake inayojulikana kama ‘LIFE OF KYLIE’ huku akiwa ni Miongoni mwa Macelebrity wenye Ushawishi Mkubwa kwenye Mitandao ya Kijamii duniani.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey