Sambaza

Baba Kanumba Amjibu Mama Kanumba, Amshushia Lawama Nzito

NI miaka saba imekatika tangu tasnia ya Filamu Bongo na taifa zima kwa ujumla lipate pigo la kuondokewa na aliyekuwa nguli wa uigizaji nchini, marehemu Steven Kanumba, +255 Global Radioimezungumza na Mama Kanumba, Bi. Florah Mtegoa na kudai kuwa hakumpa pesa za urithi Baba Kanumba kwa sababu alimkataa mtoto na kumtlkeza akiwa mtoto.

Kupitia kipindi cha Kata Mbuga cha Global Radio, Mama Kanumba amefunguka kwa mara ya kwanza mgogoro wake na baba Kanumba, ambao unatajwa kuwa unasababishwa na mali za mtoto wao na kudai kuwa hata hivyo alikuwa mchepuko wake tu sababu baba huyo alikuwa na mkewe na watoto, ndiyo maana alimtlekeza.

Hata hivyo, Baba Kanumba naye amepangua tuhuma hizo na kudai kuwa hakuwahi kumtelekeza mtoto. Mzee Charles kanumba mwenye maskani yake mkoani Shinyanaga amdai kuwa alikuwa akiishi na Kanumba tangu akiwa mdogo hata ndugu zake wanamfahamu vizuri.

Aidha, Baba Kanumba amesema hakufika msibani kwa sababu alikua akiumwa wakati msiba huo ulipotokea lakini alituma ndugu zake na walifika. Mze huyo amenda mbali zaidi na kumshushia tuhuma mpya mzazi mwenzake huyo akidai kuwa amekuwa akiomba rambirambi hadi kwnye baa na kumbi za starehe.

Pakua App ya +255 Global Radio ili Kusikiliza Vipindi vyetu, Bofya HAPA KUINSTALL APP 

BABA KANUMBA AJIBU : ” Mama Kanumba Anaomba Rambirambi Kwenye Kumbi za Starehe “

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey