Sambaza

Mama Kanumba Atamani Sana Kumrudisha Wema Sepetu kwa Mungu

MAMA wa aliyekuwa staa wa Bongo Movie, marehemu Steven Kanumba, Bi. Flora Mtegoa, amesema anatamani kukutana na malkia wa tasnia hiyo, Wema Sepetu,  ili amshauri baadhi ya mambo kuhusu maadili, kumrudia Mungu na aachane na mambo ya mitandaoni na wanaume.

Amesema hayo juzi Jumatatu wakati akipiga stori ndani ya kipindi cha Kata Mbuga cha +255 Global Radio na kusema kuwa anampenda sana Wema kwani ni miongoni mwa wasanii ambao hajawahi kukwaruzana nao tangu kifo cha mwanaye, Steven Kanumba.

Kuhusu Wema Sepetu

“Sina tatizo na Wema Sepetu, nampenda kwa moyo wangu wote, ni mwanangu, nashindwa hata kumwelezea, ninamuombea kwa Mungu ambadilishe, namuomba ajizatiti kwenye dini, hata nikikutana naye akiwa na shilingi moja huwa anatamani angalau aivunje nichukue nusu na yeye nusu.

Kama kweli yanayozungumzwa ni ya kweli, (kuhusu kuposti picha za ngono mtandaoni), namuomba asirudie, natamani angalau nikae naye nizungumze naye nimshauri.

Kuhusu Steve Nyerere

“Steve Nyerere yule ni mwanangu, nampenda sana na nitaendelea kumpenda, lakini namshauri ikitokea kuna jambo lolote la wasanii aniambie mimi nipo tayari kushirikiana nao hata kwa mawazo na ushauri.

Kuhusu Ray Kigosi (aliyekuwa swahiba wa Kanumba)

“Ni miaka minne au mitano sasa hatujaonana wala hatuwasiliani, lakini hatuna ugomvi.”

Anayamudu vipi maisha

“Mimi ni mpambanaji, ikipita nyanya au mchicha nauza, siwezi kutegemea mtu kwa sababu nina nguvu, zikitokea scene (fursa za kushiriki uigizaji) za muvi nacheza kwa sababu naweza na nina kipaji.”

Malalamiko ya wasanii (kuhusu Mtegoa) kuwapiga mizinga

“Hakuna msanii aliyewahi kunisaidia tangu mwanangu afariki, ni mwaka wa saba sasa, labda wanatafta kiki. Kwanza sionani nao labda kwenye misiba tu.”

Kipi anakikumbuka zaidi kwa Kanumba?

“Na-miss  vitu vingi sana; uwepo wake, upendo wake,  waliojifanya ni marafiki zake leo wala huwaoni. Mwanangu tulizika mwili lakini roho yake ipo na bado inaishi. Kanumba hajamchagua mtu wa kumrithi, mimi huenda nalazimisha tu kuchagua watu wa kumrithi lakini yeye hajapata.

“Ikikaribia siku ya kumbukumbu ya kufa Kanumba huwa naumia sana, wakati anakufa nilikuwa na kilo 95 lakini ziliporomoka hadi kilo 40. Nashukuru kwa sasa nimeanza kunenepa kidogo. Kanumba alikuwa hawezi kufanya chochote bila mimi. Sasa hivi Kanumba The Great tunarudi upya,  kuhusu muvi,  maudhui ya kidini (tukiwa) na mdogo wake Seth.

“Serikali na Steps Entertainment wamechukua jukumu la kuandaa documentary kwa ajili ya maisha halisi ya Kanumba alivyoishi wakati wa uhai wake. …Baba Kanumba nimekusamehe lakini hili liwe fundisho kwa wanaume wengine ambao hutelekeza watoto wao. Na wewe ungezungumzia kuhusu documentary na mwanao, usisubiri tu mtonyo,” amesema Mama Kanumba.

Pakua App ya +255 Global Radio ili Kusikiliza Vipindi vyetu, Bofya HAPA KUINSTALL APP 

Tazama Video Nzima Alipofanya Interview na +255 Global Radio

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey