Sambaza

Mitandao ya Facebook, Instagram na Whatsapp Yakumbwa na Matatizo

MITANDAO maarufu duniani ya Instagram na Facebook na WhatsApp imekumbwa na tatizo la kuwa chini dunia nzima ambapo baadhi ya watumiaji wameeleza kushindwa kupakia picha na video, huku wengine wakisema hawawezi kuperuzi picha.

 

Kupitia ukurasa wao, Instagram wamekiri kutoka kwa tatizo hilo na duniani kote na kusema wanalishughulikia lakini imeonekana kuwa ni tatizo linalotokea mara kwa mara. Ikumbukwe kuwa, mwezi Juni mwaka huu, Instagram ilipatwa na matatizo kama haya kwa baadhi ya maeneo duniani kwa muda wa saa 3, lakini hali ilirejea kama kawaida baada ya tatizo hilo kutatuliwa.

Baadhi ya mamlaka zinazosimamia masuala ya teknolojia nchini Marekani zimesema kuwa, tatizo hilo huenda likawa limesababishwa na matatizo kwenye server za Cloud Flare ambazo hutunza data na machapisho ya watumiaji wa mitandao hiyo kwani jana Jumanne, Cloud Flare walikuwa na tatizo kwenye mifumo yao ya utunzaji data.

 

Updates, Julai 4: Tayari mitandao ya Instagram, Facebook na WhatsApp imereja hewani kwa asilimia 100 na watumiaji wake wanaweza kutumia vizuri kama mwanzo baada ya timu ya watalaam kufanikisha kudhibiti tatizo lililokuwa limeikumba mitandao hiyo kwa siku nzima ya jana, amesena Msemaji wa Instagram na kuwaomba radhi watumiaji wa mitandfao hiyo dunaini kote kwa kilichotokea.

EXCLUSIVE INTERVIEW: OMAWUMI Kutoka NIGERIA na +255 Global Radio

Pakua App ya +255 Global Radio ili Kusikiliza Vipindi vyetu, Bofya HAPA KUINSTALL APP

 

Source : The Sun

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey