Sambaza

Omawumi, Meneja Wa Wizkid Watambulisha EP Mpya Global Radio

Staa anayekimbiza katika gemu la muziki nchini Nigeria, Omawumi Megbele ‘Omawumi’, akizungumza kupitia radio janja ya +255 Global Radio leo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

KIMATAIFA! Ndivyo unavyoweza kusema kwa lugha rahiiisi baada ya staa anayekimbiza katika katika gemu la muziki nchini Nigeria, Omawumi Megbele ‘Omawumi’ sambamba na meneja wa staa wa muziki, Wizkid, Mr. Sunday kutinga ndani ya viunga vya Global Group, Sinza-Mori jijini Dar na kutambulisha albamu ya nyongeza (EP).

Akizungumza kupitia radio janja ya +255 Global Radio, Omawumi alisema EP hiyo inaitwa In Her Feelings ikiwa na jumla ya nyimbo saba ambazo ni Without You, For My Baby, Mr Sinnerman,  Away, True Loving, Tabansi  na Green Grass.

“Ujio wangu Tanzania kwanza ni kutambulisha EP ya In Her Feelings lakini pia kufanya kolabo na msanii mkubwa. Nimeanza kutengeneza naye wimbo jana (Jumanne) na leo (Jumatano) nitamalizia naye.  Jina la msanii na wimbo itakuwa sapraiz mpaka itakapotoka,” alisema Omawumi.

Staa huyo pia alielezea safari yake ya muziki kuwa aliianza rasmi mwaka 2007 katika shindano la vipaji vya kuimba lijulikanalo kama Idols West Africa ambapo alikuwa mshindi wa kwanza huku akiwa na rekodi ya kushika tuzo mbili kupitia kipengele cha Best Vocals.

“Nilishawahi pia kushiriki katika Projekti ya Malaria  nchini Kenya na kuimba wimbo wa Kiswahili wa Malaria (anaimba) ‘Twaangamiza Malariaaaa’.”

Kupata mahojiano kamili tembelea tovuti ya www.globalradio.co.tz au unaweza kupakua APP yake kwa kuingia kwenye Playstore na kutafuta 255 Global Radio kupitia simu yako ya mkononi.

Pakua App ya +255 Global Radio ili Kusikiliza Vipindi vyetu, Bofya HAPA KUINSTALL APP

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey