Sambaza

Wema Aachiwa huru, Akamatwa na Kupelekwa Polisi Centro

MSANII wa filamu nchini, Wema Sepetu, amezua kizaazaa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akigoma kukamatwa na askari baada ya mahakama hiyo kumwachia huru na kisha askari kumkamata tena na kumweka mahabusu ya mahakama hiyo.

Wakati askari wakimkamata kwa nguvu, Wema aligoma kukamatwa, hali iliyosababisha mvutano kwa muda kati ya askari na mawakili wake, Albert Msando na Reuben Simwanza.

Hata hivyo, askari hao walifanikiwa kumkamata msanii huyo aliyetoka Mahabusu ya Gereza la Segerea Juni 24, mwaka huu ambapo alifika mahakamani asubuhi kwa ajili ya kusikiliza kesi yake inayoendelea mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.

Wakili wa Serikali, Glory Mwenda,  alidai hana shahidi baada ya shahidi aliyemuandaa, Koplo Safi,  kudai ni mgonjwa. Hoja hiyo ilipingwa na Wakili wa Wema, Albert Msando,  kwa madai kwamba haina mashiko, kwa vile mahakama ilishatoa ahirisho la mwisho,  hawawezi kuahirisha tena.

“Mheshimiwa shauri lipo zaidi ya siku 60, upande wa mashtaka wameshindwa kuleta mashahidi, tunaomba chini ya kifungu namba 225(5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai sura ya 20 mshtakiwa aachiwe huru,” alidai.

Wakili Mwenda alipinga akidai sheria ya siku 60 inatumika pale tu ambapo upelelezi haujakamilika, hivyo aliomba kesi iahirishwe.

Hakimu Kasonde alisema anakubaliana na maombi ya upande wa utetezi, sheria hiyo inatumika wakati wowote, hivyo mahakama inamuachia huru mshtakiwa.

Mrembo huyo wa Tanzania mwaka 2006 aliyefika mahakamani hapo leo Alhamisi Julai 4, 2019 anakabiliwa na mashtaka ya kurekodi video ya ngono na kuisambaza katika mitandao ya kijamii.

Juni 24, 2019 mahakama hiyo ilimuonya Wema kutokukiuka masharti ya dhamana, vinginevyo haitasita kumfutia dhamana yake.

UPDATE: Baada ya kuwekwa mahabusu ya Mahakama ya Kisutu, Wema alipelekwa katika kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam (sentro).

Taarifa zilizotufikia punde zimeeleza kuwa tayari Wema ameshaachiwa kwa dhamana.

Kupata Matangazo ya +255 Global Radio, Kupata Exclusive Interviews na Burudani Kibao, BOFYA LINK HII ILI KUPAKUA APP YA GLOBAL RADIO

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey