Sambaza

Kanye West Aamua kumuomba Msamaha Jay Z Hadharani

Mashabiki wa muziki wa Kanye west wamehoji kwanini amemuomba msamaha rapa mwenzake Jay Z, kwenye ngoma yake mpya ya “brothers” ambayo amemshirikisha Charlie Wilson.

Mashabiki hao wamehoji baada ya kuisikiliza na kusoma maandishi yaliyopo katika ngoma hiyo , ambayo yalikuwa yanamlenga rapa Jay Z.

Maandishi ya ngoma hiyo yanasomeka kama, “nisamehe kwa kukupoteza , nakubali kwamba nimekukumbuka ,nimekukumbuka kwenye ile familia yetu na undugu wetu, nimekumbuka kusafiri na ndege na wewe kwenda jijini Paris na kukumbatiana , na kupokea simu yako ukinipigia“.

Kanye west na Jay Z wameshafanya kazi pamoja kupitia album ya “Watch The Throne” ya mwaka 2011 na kutoa ngoma kali kama Otis, n**s in paris , No church in the wild na Welcome to the jungle.

Wawili hao kwasasa hawana ukaribu kama ule wa mwanzo , na hawajaonekana wakiwa pamoja kwa muda mrefu hivi sasa baada ya Vita ya chini chini ya maneno aliyoianzisha Kanye West baada ya Jay Z Kufanya Wimbo wa Pamoja  na Justin Timberlake ‘Suit & Tie’ ambao Kanye West aliudiss na Kusema kuwa wimbo huo sio mzuri na hauendani na Jina lake lilivyo Kubwa. 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey