Sambaza

7 Wafariki kwa Ajali wakielekea Chato, Watano ni Wafanyakazi wa Azam Tv

WATU saba wakiwemo wafanyakazi watano wa kampuni ya Azam Media wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori, uongozi wa Azam Media umethibitisha.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Julai 8, 2019 eneo la Shelui mkoani Singida wakati wakieleleka wilayani Chato Mkoa wa Geita katika uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Chato-Burigi.

Taarifa kutoka katika kampuni hiyo zinaeleza kuwa wafanyakazi hao walikuwa katika gari aina ya Coaster na kwamba madereva wawili wa magari hayo nao wamefariki dunia. “Katika basi hilo dogo wafanyakazi walikuwa kumi, watano wamejeruhiwa,” zinaeleza taarifa hizo.Uzinduzi wa Hifadhi hiyo unafanyika kesho Jumanne Julai 9, 2019 na Rais wa Tanzania, John Magufuli. Inadaiwa waliofariki ni watano wa Azam na madereva wawili wa coaster;

Said Haji – Camera

Charles Wandwi -Camera

Salim Mhando – Switcher

Florance Ndibalema- Sound

Kasongo – Engineer

Majeruhi ni;

Said Mwinshehe- Camera

Masawe-Engineer

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey