Sambaza

Chris Brown Azidi Kuandamwa, Kuburuzwa Mahakamani na Mzazi Mwenzie

Staa wa Muziki Duniani Chris Brown, amezidi kuandamwa na misukosuko baada ya mzazi mwenzie, Nia Guzman kumfungulia mashtaka Mahakamani baada ya Brown Kugoma kutoa Pesa ya Matunzo ya Mtoto.

Nia Guzman ambaye ana mtoto mmoja na Chris Brown aitwae Royality, amemfungulia kesi staa huyo kwa kosa la kutotoa pesa za  matumizi kwa mtoto na amesema amefungua mashtaka hayo baada ya kuona Chris Brown amegoma kulipa shilingi milioni 40 alizoambiwa alipe na mahakama mwezi wa pili mwaka huu.

“Huwa hashiriki katika kutoa msaada wa matumizi ya mtoto wake na gharama zimeongezeka, huwa anapuuza matangazo yanayotolewa na mahakama katika suluhisho ya malezi ya mtoto. Nataka kurejeshewa gharama zangu zote nilizokuwa natoa tangu mwanzo wa kesi, pia alipie thamani ya nyumba aliyokubali kulipa, jumla nataka milioni 592”.

Mbali na kesi hiyo mama huyo amesema kuwa anahitaji malipo ya Shilingi milioni 15 kwa kila mwezi kwa matumizi ya mtoto huyo, Ingawa Chris Brown aliwahi kulalamika kuwa mama mtoto huyo huwa anaongeza pesa kwa ajili ya matumizi yake binafsi.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey