Indigo Ya Chris Brown Imeshika Namba Moja Kwenye Chart Za Billboard
MWANAMUZIKI Chris Brown anazidi kuvunja rekodi ya kuwa msanii aliyeuza nakala nyingi za Album yake ya Indigo wiki iliyopita , Album iyo imefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye chart za Billboard 200.
Album ya Indingo imefanikiwa kuuza kopi 108,000 ndani ya wiki ya kwanza, kwa Chris Brown hii ni Album yake ya tatu kushika namba moja kwenye chart za Billboard ukiachana na Album yake ya mwaka 2012 F.A.M.E na ya 2012 Furtune pia ni Album yake ya 10 kuingia kwenye orodha 10 ya chart za Billboard.
Hii ndio orodha ya Album 10 zilizouza kopi ndani ya wiki hii
1. Chris Brown – Indigo – 108,000
2. Lil Nas X – 7 – 62,000
3. Billie Eilish – When We All Fall Asleep, Where Do We Go? – 52,000
4. The Black Keys – Let’s Rock – 52,000
5. Chance the Rapper – Acid Rap – 40,000
6. Khalid – Free Spirit – 38,000
7. Lizzo – Cuz I Love You – 36,000
8. Mustard – Perfect Ten – 36,000
9. J Balvin and Bad Bunny – Oasis – 36,000
10. Jonas Brothers – Happiness Begins – 29,000