Chin Bees na Country Boy Wazidi kutunishiana Misuli
Wanamuziki wa Bongo wa Miondoko ya Trap wanaofanya vizuri kwenye game ya Muziki, Country Boy na Chin Bees wameendeleza vita ya maneno katika interviews wanazofanya huku kila mmoja akivimba kuwa ni bora zaidi ya mwenzake.
Akifanya Interview na kipindi cha E News kinachorushwa na kituo cha EATV, Country Boy amemjibu Chin Bees ambaye amewahi kukaririwa akisema kuwa Country sio levo zake, na amemzidi mbali sana. Country Boy amesema “Chin Bees ana tatizo na mimi, ananitafuta kwa sababu nafanya kazi ambazo zinaonekana zinamgusa, ni mdogo wangu nimemsaidia mimi katika ‘game’, hanifikii kwa kurap, kuvaa hata maisha“, amesema Country Boy.
Country Boy ameenda mbali zaidi na kusema kuwa bila yeye Chin Bees asingetoka kwa sababu amemsaidia vitu vingi hadi kuandika baadhi ya nyimbo zake.