Chris Brown Na Mzazi Mwenzake Wayamaliza Kuhusu Malezi Ya Mtoto Wao
MWANAMUZIKI wa miondoko ya RnB Chris Brown pamoja na mzazi mwenzake Nia Guzman baada ya kuwa na mvutano muda mrefu kwenye swala la malezi ya mtoto wao Royalty sasa wameamua kukaa chini na kuelewana .
Nia Guzman amaekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kudai pesa za malezi ya mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitano kutaoka kwa mzazi mwenzake Chris Brown na amethibitisha kua kwa sasa wapo kwenye maelewano mazuri
Mtandao The Blast mwenzi February ulilipoti kuwa Chris Brown alitakiwa kutoa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 40 za kitanzania kwa ajili ya malezi ya mtoto wao lakini hakufanyahivyo ila Gumza amekanusha taarifa izo na kusema sio za kweli kwani kwa sasa wamemaliza kesi yao na wapo vizuri.
Nia Guzman mwaka 2017 alifungua mashtaka dhidi ya Chris Brown kuhusu Malezi ya mtoto wao lakini baadae Mahaka ya California inchini Marekani ilitupilia mbali kesi iyo.