Sambaza

Uchebe Amponza Shilole

MUME wa mwanamuziki na muigizaji wa filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ Ashiraf Uchebe amemponza mkewe huyo baada ya kuzuiliwa kuingia katika Ukumbi wa Mlimani City katika sherehe ya kuzaliwa kwa mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘mama Dangote’.

Iko hivi; katika siku hiyo ambayo mastaa wengi walialikwa kuhudhuria, Shilole alifika hapo akiwa na Uchebe lakini baada ya kufika, walinzi walidai kuwa hawamtambui Uchebe hivyo aingie peke yake.

Kutokana na maneno hayo, hayakumfurahisha Shilole na kuanza kumtetea kwa kutoa maneno makali akidai kwa nini mumewe adharaulike angali yupo.

“Tena mnikome kabisa, sipendi tabia ya kumdharau mume wangu,” alisema Shilole na kuanguka chini baada ya kukanyaga gauni lake ambalo lilikuwa refu. Hata hivyo, baadaye wawili hao waliachiwa kuingia ndani kujumuika na wenzao.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey