Sambaza

Aika na Nahreel Wamuonyesha ‘Jamaika’ Hadharani

Miongoni mwa Couple ya Wasanii iliyodumu kwa muda mrefu hapa Bongo ni ya Aika na Nahreel ambao wanaunda kundi la Muziki la Navy Kenzo. Licha ya kufanikiwa kimahusiano, pia wamefanikiwa kimuziki ikiwa ni kundi ambalo linafanya vizuri ndani na nje ya mipaka ya Tanzania, Navy Kenzo kwa nyakati tofauti wamefanikiwa kutoa hit songs kama ‘Katika’ Waliofanya na Diamond Platnumz, Game, Kamatia, Fella na nyingine nyingi ambazo zinafanya vizuri mpaka leo.

Couple hiyo ambayo wana mtoto Ajulikanaye kama ‘Gold’ wamefanikiwa kupata mtoto wa pili waliyempa jina ‘Jamaika’. Baada ya kujifungua Aika na Nahreel hawakumpost Jamaika Kwenye Mitandao ya Kijamii na wamefanya hivyo kwa mara ya kwanza kwa kuweka picha yake kwenye mtandao wa Instagram hivi karibuni.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey