Moni Centrozone : “Sitabiriki kama Wasanii Wengine “
RAPA kutoka Majengo Sokoni jijini Dodoma anayekimbiza kunako gemu la Muziki wa Hip Hop Bongo, Moni Centrozone ametoa siri ya kutotabirika katika gemu. Akizungumza Leo katika Kipindi cha Bongo 255 kupitia +255 Global Radio Moni anayetikisa na Ngoma ya Mtiti alisema amekuwa hatabiriki kwenye nyimbo zake nyingi kutokana na kutofanana na wasanii wenzake ambao wanafanya muziki huo.
“Ukiangalia muziki wangu hautabiriki, wimbo niliofanya na Mr T Touch siyo wa mapenzi, mtiti siyo mapenzi. Nafikiri umeona jinsi muziki ulivyo rahisi kupenya na wa biashara. Mtu anapoambiwa muziki wa biashara anajua mapenzi mwanzo mwisho na ndiyo maana kuna msongamano kubwa sana katika gemu hili.
Moni Aliongeza
“Ukisikiliza ngoma yangu kama Mihela ina topic mwanzo mwisho, ukisikiliza nyingine ya Chuchu Dede nayo ni mapenzi lakini inamsifia msichana aliyejitunza hadi anaonekana.
“Ninapoandika mistari kwanza nakuwa na picha mbili ya kwanza nikiwa katika mahusiano na pili nikiwa kama Moni msanii. Ngoma ya Mihela inamgusa kila mtu ambaye aliteleza katika mapenzi na kuja kufanikiwa hapo baadaye. Kuna waliofanikiwa hawapo na watu wao wa zamani na wengine wametoka na watu wao kutoka chini hadi juu.”
Imeandaliwa; Andrew Carlos/GPL