Sambaza

Baraka the Prince Akimbia Bongo, Aeleza Sababu

Msanii wa Muziki wa Bongofleva nchini Baraka the Prince, Amehamishia makazi yake nchini Kenya na Kutoa sababu za kufanya maamuzi hayo. Akipiga story na moja ya kituo cha televisheni hapa Bongo, Baraka Amefunguka;

“Kwa kweli nina makazi Kenya, nina makazi hapa , sijakimbia Tanzania bado nina familia hapa, nina nyumba na ninaishi hapa. Nimeenda Kenya kwa sababu nataka kutanua wigo na soko la muziki wangu, nataka soko langu liwe kubwa kwa Afrika mashariki”

Pia amefunguka kuhusu tetesi zilizokuwa  zikisambaa mitandaoni kuwa hivi sasa amekuwa tapeli, baada ya kudaiwa kumtapeli Msanii mwenzie wa kike Sex Dinah.

“Hivo vitu vinatokea kwa sababu mimi ni mtu maarufu, sio mimi tu hata wanasiasa wakubwa, mabilionea nao wanaitwa matapeli, kwahiyo hamna kitu chochote kilichokuwa kinaendelea kati yangu mimi na ile stori iliyokuwepo” .

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey