Shawn Rhoden Atuhumiwa kwa Ubakaji, Asakwa
Mwanamke aliyemfungulia mashtaka ni mtunisha Misuli mwenzie ambaye anadai alifanyiwa kitendo hicho cha udhalilishaji na Shawn mwaka 2018.
Taarifa kutoka Mamlaka za Mji huo zinasema kuwa Shawn (44) bado hajatiwa mbaroni lakini hati ya kukamatwa kwake imeshatolewa na Muda wowote atatiwa mbaroni. Kulingani na nyaraka za mahakama zilizodukuliwa na mtandao wa TMZ, Mlalamikaji huyo anadai kufanyiwa kitendo hicho alipokwenda kumtembelea Shawn kwenye chumba cha hotel, na alimchukulia Shawn kama mentor wake hivyo hata alipomwalika hotelini hakuwa na wasiwasi.
Ripoti kutoka ndani ya jeshi la polisi zinasema kuwa Uchunguzi wa daktari umekwisha fanyika na sampuli za DNA za Shawn na Mlalamikaji zimeonyesha kuwa ni kweli Shawn alifanya kitendo hicho.
Toa Maoni Yako Hapa