Sambaza

Queen Mugesi atwaa taji la Miss Kinondoni 2019

USIKU wa kuamkia Julai 13 lilifanyika shindano la kumsaka Miss Kinondoni katika ukumbi wa Life Park Mwenge, ambapo mlimbwende Queen Mugesi Aynory (19) ameibuka kidedea na kuvaa taji lililokuwa linashikiliwa na Queenelizabeth Makune.

Mshindi wa pili alikuwa Prisca Kisunda, watatu Leila Adim wa nne Queen Anthony na wa tano ni Flaviana Steven.

Awali alianza kupanda jukwaani msanii wa Bongo Fleva anayefahamika kwa jina la Bi. Aisha ambaye aliimba nyimbo kadhaa, kisha mshereheshaji (MC) aliwakaribisha washiriki wa Miss Kinondoni 2019 jukwaani kwa ajili ya kuwaburudisha wageni waalikwa sambamba na kuonesha mavazi yao.

Miongoni mwa mavazi yaliofunika usiku huo kwa washiriki ni pamoja na mavazi ya ubunifu, ufukweni na mwisho mavazi ya mtoko (usiku).

Mbali na kumpata mshindi wa Miss KinondonI 2019, vile vile washindi wa Categories mbalimbali kama vile Miss Photogenic, Miss talent, top model na miss personality walitangazwa. Mshiriki namba 3, Christina Andrew alishinda taji la Miss talent, Prisca Kisuda ambaye alishika namba mbili Miss Kinondoni pia alishinda taji la Top Model, huku Christina Anold akishinda taji la Miss photogenic na Leah Geofrey akiibuka Mshindi wa Miss Personality.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey