Sambaza

Vanessa Mdee Alamba Shavu la Maana Kenya

Bongo Fleva diva Vanessa Mdee amelamba shavu la kuwa mmoja wa majaji wa shindano la kutafuta vipaji la Afrika Mashariki (East Africa’s Got Talent) .

Katika safu ya Majaji watakaofanya kazi na Vanessa katika shindano hilo, wapo pia Gaetano Kagwa ambaye ni mtangazaji wa Capital Radio nchini Uganda (Aliwahi pia kushiriki shindano la Big Brorher Africa), Mwingine ni DJ Contact Makeda kutoka Rwanda, pamoja na Mtangazaji maarufu nchini Kenya Jeff Koinange.

Vile vile Host wa show hiyo ambayo imepangwa kuanza mwezi August Mwaka huu, atakuwa ni mchekeshaji kutoka Uganda, Anne Kansiime. Show hiyo itafanyika nchini Kenya na wasshiriki kutoka nchi za Afrika Mashariki watakutana na kuchuana kuwania kitita cha Shilingi za Kitanzania Milioni 100.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey