Sambaza

Irene Uwoya, Steve Nyerere Waitwa BASATA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza amesema kuwa wameamua kumuita msanii wa filamu nchini, Irene Uwoya pamoja na Steve Nyerere, kufuatia kitendo alichokifanya Irene cha kuwarushia pesa waandishi wahabari katika mkutano wa wasanii, uliofanyika Julai 15, Dar

Akiongea leo Julai 17, Godfrey Mngereza amesema kufuatia wito huo, wao kama Baraza hawajapanga kuwachukulia hatua zozote zile za kisheria wasanii hao.

”Wajibu wa baraza ni kukaa na wasanii, halafu kuzungumza nao, na baraza linafanya kazi kwa mujibu wa sheria lililoziweka na kama uliona yale ni masuala ya fedha”,  amesema Mngereza.

Aidha kwa upande wake Steve Nyerere amekiri kupokea taarifa hizo na kwamba yeye kama msanii na BASATA ni Serikali, hivyo atafika kama alivyotakiwa.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey