Amanda Giovacco Amefungua Kesi Ya Madai Dhidi Ya Drake
MWANADADA Amanda Giovacco mwenye umri wa miaka 24 amefungua kesi ya madai ya kupata madhara ya ubongo kwenye show ya rapa Drake
Amanda alisema siku ya August,8, 2016 katika onyesho la Madison Square Garden, Drake alipiga show live mashabiki walifanya fujo hadi kurusha chupa za vinywaji na moja ilimpiga kichwani na kupelekea kupata madhara.
Amanda aliendelea kusema show hiyo haikuwa na ulinzi wa kutosha na kupelekea fujo nyingi kufanywa na mashabiki, pamoja na pombe kali zilikua kwa wingi na walinzi walishindwa kumudu umati wa watu na fujo za show za Drake. Matatizo aliyopata ya ubongo yamepelekea Amanda kushindwa kwenda kusomea udaktari.
Toa Maoni Yako Hapa