R. Kelly Akana Mashtaka Arudishwa Rumande
MWANAMUZIKI R. Kelly baada ya kukaa jela kwa siku tano jana julai 16 amepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka 13 ya Kingono R. Kelly aliingia mahakamani akiwa amevaa mavazi ya wafungwa rangi ya machungwa miguuni akiwa amefungwa pingu.
Mahaka imemnyima dhamana na amerudishwa rumande huku kesi zake zikiendelea kufanyiwa uchunguzi. Wakili wa serikali amesema R. Kelly hakutakiwa kupewa dhamana sababu ni mtu hatari kwa jamii, haswa kwa watoto wadogo wa kike, tunaogopa atashawishi mashahidi na kushawishi mabadiliko ya kesi hii. Lakini Wakili wa R. Kelly, Steve Greenberg amesema mteja wake hana mpango wa kukimbia nchi yake sababu hana sababu wala hela za kufanya hivyo.
Wapenzi wawili wa R Kelly, Joycelyn Savage na Azriel Clary wanaoishi nae katika nyumba yake kwenye jengo la Trump Tower mjini Chicago walikuwa mahakamani kumtia moyo mpenzi wao. Fahamu akikutwa na hatia kwenye makosa haya R. Kelly anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 195 jela na labda miaka zaidi mjini New York.