Sambaza

R. Kelly Akana Mashtaka Arudishwa Rumande

Image result for r. kelly

MWANAMUZIKI R. Kelly baada ya kukaa jela kwa siku tano jana julai 16 amepandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka 13 ya Kingono R. Kelly aliingia mahakamani akiwa amevaa mavazi ya wafungwa rangi ya machungwa miguuni akiwa amefungwa pingu.

 

Related image

Mahaka imemnyima dhamana na amerudishwa rumande huku kesi zake zikiendelea kufanyiwa uchunguzi. Wakili wa serikali amesema R. Kelly hakutakiwa kupewa dhamana sababu ni mtu hatari kwa jamii, haswa kwa watoto wadogo wa kike, tunaogopa atashawishi mashahidi na kushawishi mabadiliko ya kesi hii. Lakini Wakili wa R. Kelly, Steve Greenberg amesema mteja wake hana mpango wa kukimbia nchi yake sababu hana sababu wala hela za kufanya hivyo.

Image result for r. kelly Joycelyn Savage and Azriel Clary

Wapenzi wawili wa R Kelly, Joycelyn Savage na Azriel Clary wanaoishi nae katika nyumba yake kwenye jengo la Trump Tower mjini Chicago walikuwa mahakamani kumtia moyo mpenzi wao. Fahamu akikutwa na hatia kwenye makosa haya R. Kelly anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 195 jela na labda miaka zaidi mjini New York.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey