Sambaza

AY Azungumzia Kuvunjika kwa Ndoa Yake

Msanii Legend wa Bongofleva, Ambwene Yessaya (A.Y) amefunguka kuhusu tetesi zilizoanza kuenea kwa kasi kuhusu Kuvunjika kwa ndoa yake na Remmy, binti kutoka Rwanda ambaye walifunga naye ndoa Miezi Kadhaa iliyopita na Kufanikiwa Kupata nae Mtoto Mmoja, Aviel.

Tetesi za kuvunjika kwa ndoa yao zilianza kusambaa kwenye Mitandao ya Kijamii hapa Bongo, na Alipoulizwa na Kituo kimoja cha televisheni kuhusu tetesi hizo, AY alisema :

Hizo story gani sasa, wewe za udaku mimi sio mtu wa mambo ya udaku. Hizi stori za udaku mimi nazitoleaje ufafanuzi, kwasababu mtu mmoja anaamka nakuandika anachotaka,” 

Alifunguka AY akigoma kabisa kulizungumzia hilo suala. Tetesi hizo zilizosambaa kwa kasi hapa bongo zinasema kuwa, Remmy aliingia tofauti na AY na kuamua kuondoka nchini na kumuachia mtoto AY.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey