Sambaza

Kim Kardashian Aendelea Na Kampeni Ya Kusaidia Wafungwa

Image result for kim kardashian

MWANAMITINDO maarufu duniani Kim Kardashian kupitia ukurasa wake wa Instagram aliweka picha akiwa kwenye Video Call na jamaa mmoja aliyefahamika kama Kevin Keith ambaye kwa mujibu wa Kim, Kevin alihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 1994 kwa kosa la kuwaua wanawake wawili na binti mdogo wa miaka Minne.

Imeelezwa kuwa polisi hawakufanya mahojiano na Keith, bali walimkamata tu na kumfikisha mahakamani. Hakuna ushahidi wowote wa mauaji hayo uliopatikana. Keith aliendelea kudai hana hatia lakini alihukumiwa kifungo cha maisha.

Kim Kardashian ambaye hivi karibuni amekuwa akijikita sana na masuala ya sheria na kuwasaidia wafungwa mbali mbali ameandika kuwa amemsikiliza kwa makini na anatamani dunia isikie kilichomtokea. Pia amesema umepatikana ushahidi wa kutosha na haki itatendeka.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey