Sambaza

Victoria Kimani Amshushia Lawama Beyonce

Victoria Kimani ameeleza kusikitishwa kwake baada ya kuona hakuna hata msanii mmoja wa Kenya na kutoka Africa Mashariki kuwepo kwenye Album mpya ya  Beyonce “The Lion King: The Gift”, ambayo Album hiyo amewapa mashavu zaidi wasanii wanaotokea nchini Nigeria.

Victoria Kimani ali-tweet kwa kuandika “Filamu imebeba misingi ya nchi ya Kenya sawa, lakini Malkia wetu ametusahau sisi wa Kenya na wana Africa Mashariki, Sisi hatujawakilisha katika Album yake, inauma sanaa ni hivyo tu” ameandika Victoria Kimani.

Julai 16, Beyonce aliutangazia Ulimwengu ujio wa  Album yake mpya ambayo ndani ya Album hiyo ameshirikisha wasanii kutokea barani Africa ambao ni Wizkid, Tekno, Burna Boy, Mr Eazi, Yemi Alade, Tiwa Savage wote hawa wanatokea nchini Nigeria, pamoja na Shatta Wale kutokea nchini Ghana.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey