Sambaza

“Niliparamia Wanawake kweli kweli ” Diamond Afunguka

Msanii ambaye hakosi kwenye headlines za magazeti, Mitandao ya kijamii pamoja vyombo mbalimbali hapo Bongo, Diamond Platnumz amefunguka kuhusu jinsi gani amenusurika kupata magonjwa ya zinaa kutokana na tabia yake ya ‘Kuparamia’ wanawake.

Akiongea mbele ya wanachuo na Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh. Aggrey Mwanri, Diamond Platnumz ambaye hivi sasa ni balozi wa TACAIDS, amesema

“Mimi niliparamia mambo kweli kweli ila Mungu akaninusuru sana, niliparamia kweli kweli. Lakini nikapenya kwenye tundu la sindano sasa hivi nimeamua kutulia kwa Tanasha, na sitaki kabisaa kurudia yale mambo”

Diamond Platnumz na ‘timu’ nzima ya Wasafi pamoja na wasanii wengine kibao walikuwa Mkoani Tabora kwenye Tamasha la Wasafi festival, ambalo linaloendelea kufanyika katika baadhi ya Mikoa hapa Tanzania.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey