Sambaza

“The Lion King” ya Beyonce yamuibua Vanessa Mdee

Filamu ya ‘The Lion King’ ameendelea kuzua gumzo hususani katika nchi za Afrika Mashariki baada ya wasanii wengi kutoa lawama zao kwa kutokushirikishwa katika album ya filamu hiyo. Maudhui ya kimandhari  ya filamu hiyo yamehusisha uasilia wa nchi za Afrika Mashariki, lakini wasanii kutoka Afrika waliopewa shavu katika filamu hiyo ni wa Afrika Magharibi. Katika album ya Filamu hiyo, Beyonce ameshiriki kwa Asilimia kubwa zaidi na wasanii wa Afrika Mashariki wamekuwa wakimtupia Lawama yeye.

Wasanii kutoka Kenya walionyesha kutokuridhishwa na jambo hilo, na aliyeanza kutoa ya moyoni alikuwa ni Msanii Victoria Kimani Aliyeandika akionyesha kutokuridhishwa kwake.

Soma Hapa : Victoria Kimani Amshushia Lawama Beyonce

Msanii Mwingine aliyetoa ya Moyoni ni Polycarp wa Sauti Sol ambaye naye kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:

This is the Lion King ´New Africa´ Album with soundtracks of the new Lion King movie. For a movie who´s concept is fully based on the Kenyan and Tanzanian scenery, use of Swahili phrases and references, you would think they would at least consider artists from this region and not focus on artists from one country/region.

Baada ya wasanii hao Kufunguka, Msanii wa Bongo Vanessa Mdee naye aliona asikae kimya kuhusu hilo, Vanessa kupitia ukurasa wake wa Instagram pia ameandika;

Hii kitu ni biashara Poly, na waPopo wako na interests zao. Wote wanajua filamu iko set in East Africa na kihalali tungestahili kupata kanafasi, lakini hatuna wanaotuwakilisha huko kwa maExec wa Disney au kwa team ya Beyoncé. Isitoshe wakipiga mahesabu kihalali watu wa magharibi wanatuzidi kibiashara kwenye ununuzi wa bidha na mziki ndani na nje ya bara la Afrika.

Kihalali kabisa ingepaswa hii album ijae Kiswahili na masound ya pande zetu lakini kwenye soko la kimataifa bado sisi sio wazito in comparison to watu wa magharibi. Wangepaswa kufanya research to fully embody the essence of Simba. Lakini ndio hivyo. Na kiukweli ni misrepresentation na kuna matata lakini ndio hivyo soko linavamiwa. Shikeni la kwenu. Ownership.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey