Ghetto Kids Kufanya Collabo na Wiz Khalifa
Kundi la Dance la Gheto Kids la nchini Uganda linaloundwa na watoto waliokulia mtaani na kuamua kutumia Sanaa ya Dance kama njia ya kujiepusha na matendo maovu ya mtaani, Lipo nchini Marekani kwenye ziara ya kimuziki na kwa ajili ya kufanya ‘Colabo’ na baadhi ya wasanii wakubwa nchini humo.
Wakipiga story na Mtandao wa Howwe wa nchini Uganda, Gheto Kids wamethibitisha kufanya project kubwa sana na Wiz Khalifa, Swae Lee, French Montana na wasanii wengine wengi. Kundi hilo lilipata Umaarufu baada ya kushirikishwa na Eddy Kenzo katika baadhi ya nyimbo zake, pia msanii wa Marekani mwenye asili ya Morocco, French Montana aliwashirikisha katika nyimbo yake ‘Unforgettable’.
Pia wanatarajia kufanya show kubwa wakiwa nchini humo katika Tamasha la Jumuiya ya Madola (Common Wealth summit) mwezi septemba mwaka Huu.