Sambaza

Ruby Azungumzia Ndoa yake ya ‘SIRI’

Msanii wa kike anayefanya poa kwenye game ya  BongoFleva hapa nchini Tanzania Ruby, ameeleza sababu ya kumuonyesha hadharani mpenzi wake ajulikanaye kwa jina la “Kusah”, ambaye naye pia ni msanii.

Ruby ameeleza hayo baada ya kuulizwa kuhusu kumuonyesha waziwazi mpenzi wake huyo tofauti na alivyokuwa awali baada ya kuwa msiri kwa muda mrefu kwenye suala la mahusiano yake ya kimapenzi.

“Kila jambo na wakati wake, na mahusiano ambayo wewe mwenyewe ndio unajua yako vipi kwake, haihitaji kuwaonyesha watu, ila inatakiwa kama unafanya basi unafanya kweli kutoka moyoni mwako na kwa mapenzi ya kweli”.

Aidha mpenzi wake Ruby “Kusah” amedokeza kuwa suala la ndoa ni siri yao “usikute tayari tumeshafunga ndoa, lakini hata sisi tuna mambo yetu binafsi sio kila mtu ajue vitu vyetu, kwa hiyo usikute ndoa ishafungwa na kama bado hawajaona, huenda wakaona hivi karibuni”.

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey