Sambaza

Diamond Atangaza Ku ‘sign’ Wasanii Wapya WCB

Boss wa lebo inayofanya vizuri katika Muziki wa Bongofleva  Tanzania na Afrika kwa Ujumla (WCB), Diamond Platnumz ametangaza ujio wa wasanii wapya katika lebo yake ya WCB. Mpaka sasa lebo hiyo inawasimamia kwa ukamilifu wasanii Harmonize, Ray Vanny, Mbosso, Queen Darleen na Lavalava

Kupitia akaunti yake ya twitter, Diamond Platnumz ametangaza kuongeza wasanii wengine wawili katika lebo hiyo, Japokuwa amegoma kuwataja kwa majina lakini amedokeza kuwa ni Msanii wa kike na wa kiume.

Akizungumza katika moja ya Show zake za Wasafi Festival zinazoendelea kufanyika nchini, Diamond Platnumz amefunguka;

Unajua bwana mimi sikufichi sisi watu wa kimasikini na baraka twazipata tukisaidiana. tukishikana mikono wenyewe kwa wenyewe. Tumesign wasanii wengine wawili, msanii mmoja wa kike, mwingine wa kiume na naamini watu watawapenda. Tukianza kuwatoa sa hivi tutavuruga, hawatapata attention kwa sababu ya Wasafi Festival ina makelele sana. Wasafi Festival ikifanyika shughuli zote nchini hazifanyiki, labda za serikali lakaini sio entertainment, tukiwatoa sahi tutawahiribia.

 

Toa Maoni Yako Hapa
#TUMESTUKA #NAWESTUKA! Pakua App Ya >>>255 Global Radio, Bofya Hapa

spotiXtra

jerseys wholesale Danton Heinen Jersey